KAMISHNA MKUU TRA AKUTANA NA UMOJA WA MABENKI

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Yusuph Mwenda akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka umoja wa mabenki nchini leo Desemba 11,1024 jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mbali mbali amewasikiliza na  kuwashukuru kwa kuendelea kulipa kodi na kuwezesha walipakodi wengine kufanyabiashara.

Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema mwezi huu wa Disemba ni mwezi wa kuwashukuru na kuwasikiliza walipakodi wote nchini.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Yusuph Mwenda amebainisha hayo leo Desemba 11, 2024 jijini Dar es Salaam alipokutana na Umoja wa Bank Tanzania (TBA) ofisini kwake kwa lengo la kuwasikiliza na kuwashukuru kwa kuendelea kulipa kodi na kuwezesha walipokodi wengine kufanyabiashara.

Amesema, leo tumewashukuru kwa namna ambavyo wamekuwa wakifuata masharti ya kulipa Kodi, benki ni moja kati ya walipa Kodi wazuri hivyo tunawashukuru sana wote na kwa niaba yao tumewashukuru walipa Kodi wote nchini Kwa namna ambavyo wamekuwa walipa Kodi toka mwaka wa fedha ulivyoanza julaii 2024.

“Tumewasikiliza changamoto zao na tumekubaliana Kwa pamoja namna ya kuzitatua, huu ni mwezi wa kuwasikiliza na kuwashukuru walipa Kodi wote nchini, tumeanza na hawa wa mabenki tutawafikia wengine wote nchini na wengine tutawafuata kwenye shughuli zao.” Amesema Mwenda

Aidha, Kamishna Mwenda amesema yeye pamoja na menejimenti ya TRA hawatakaa ofisini mwezi huu bali watatoka kwenda kuwafuata na kuwasikiliza walipakodi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania, Geofrey Mchangila ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Citibank ameshukuru kukutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu na wameweza kujadiliana mambo mbalimbali ambayo yataendelea kuboresha sekta ya fedha na kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

“Ikumbukwe kwamba mwezi wa Oktoba tulikutana na Kamishna pamoja na Gavana wetu wa benki kuu hivyo leo Mimi pamoja na wenzangu kutoka kwenye mabenki mbali mbali tumefurahi sana”.

“Tumezungumzia masuala mbali mbali ya namna ya kuboresha ukusanyaji wa kodi hapa nchini, tumefurahishwa zaidi na jinsi kamisha alivyoweza kutambua umuhimu wa mabenki pia tumejadiliana mambo mbali mbali ambayo tunaamini yataboresha sekta ya fedha na vile vile kutoa mchango katika kukuza juhudi zetu kama sekta ya fedha kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.” Amesema Mchangila

Naye Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema TBA itaendelea kushirikiana na TRA kuhakikisha kwamba mabenki yataendelea kulipakodi sahihi na kwa wakati kwa manufaa ya nchi.

Insert Ruth Zaipuna.

“Tutaendelea kushirikiana na TRA kuhakikisha kwamba nchi ama makampuni hasa sekta ya mabenki tunaendelea kulipa Kodi sahihi na kwa wakati kwa manufaa ya nchi yetu, Kodi ni mihimu Kwa sababu inahitajika Kwa ajili ya maendeleo ya nchi.” Amesema Zaipuna.

Mamlaka ya Mapato Tanzania imedhamiria kutumia mwezi wa Desemba kuwashukuru walipakodi wote wanaoendelea kulipa kodi zao sahihi na kwa wakati hata kufanikisha mamlaka hiyo kuvuka lengo la makusanyo zaidi ya asilimia 100 kwa miezi mitano mfululizo kuanzia Julai hadi Novemba, 2024.

Related Posts