Maxime asema uzembe umewaponza kwa Singida

DODOMA Jiji jana ilipokea kipigo cha mabao 2-1 kikiwa ni cha sita katika Ligi Kuu Bara kutoka kwa Singida United, lakini kocha wa kikosi hicho amekiri wameangushwa na uzembe walioufanya wachezaji dakika 20 za mwanzo kwenye Uwanja wa Liti, mjini SIngida ulipochezwa mchezo huo.

Elvis Rupia alifunga mara mbili dakika ya nane na 15 iliyotosha kuizamisha Dodoma ambayo imesalia nafasi ya 10 ikiwa na pointi 16 baada ya mechi 14, huku Singida ikiongeza pointi na kufikisha 27 hjapo imesalia nafasi ya nne nyuma ya Yanga zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Kocha Maxime amesema katika mchezo huo waliharibu mambo mapema tu dakika 20 za mwanzo kutokana na umakini mdogo uliofanywa na safu ya ulinzi huku eneo la ushambuliaji lilikosa utulivu wa kuzamisha mipira nyavuni, licha ya kuja kulipata moja kipindi cha pili mara alipozungumza wakati wa mapumziko.

Maxime amesema timu hiyo ilitengeneza nafasi nyingi kuliko Singida, ikiwa ni nafasi nne za wazi lakini hata kukosa umakini iliwakwamisha ikizingatia walikutana na timu yenye wachjezaji wazoefu wengi.

“Yameshatokea na tunajipanga kwa mchezo ujao ili tuweze kupata matokea mazuri, kwani mechi hii ya Singida tumejiangusha wenyewe, kama tumetulia tulikuwa tuibuke na ushindi mnono tu,” amesema Maxime, beki wa kulia wa kimataifa wa Tanzania aliyewahi kuwika na Mtibwa Sugar na timu ya taifa, Taifa Stars.

Kocha huyo ameweka wazi kuwa kama mwalimu kwa kushirikiana na wasaidizi wake wanaenda kufanyia kazi makosa yote ambayo yalijitokeza katika mchezo was jana na kuwafanya kupoteza mechi ya pili mfululizo, ukiwemo ule wa mwisho dhidi ya Azam FC walipokandikwa mabao 3-1.

Alitumia fursa hiyo pia kuwaomba mashabiki wa Dodoma Jiji kuendelea kuipa sapoti timu yao huku akiwaahidi kurudi imara katika mechi zijazo na kuwapa furaha ambayo ndio wanastahili.

Related Posts