RAIS DKT. SAMIA FANYAUTEUZI, AMPANGIA KITUO CHA KAZI MMOJA

Zanzibar 13 Disemba, 2024
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na kumpangia Balozi kituo cha kazi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni:-
Bw. Majaba Shabani Magana ameteuliwa kuwa Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) akichukua nafasi ya Bi. Fatma Ayoub Mwinyimvua Simba. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Magana alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Wakubwa, Benki ya Azania; na
Balozi Selestine Gervas Kakele amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria. Balozi Kakele anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Benson Alfred Bana ambaye amestaafu.
Imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa B. Nyanga

Related Posts