Singasinga wakabidhi msaada Makao ya Watoto Faraja Mburahati

NA MWANDISHI WETU.

JAMII ya Singasinga Mkoa wa Dar es Salaam, imekabidhi msaada katika Makao ya Kulea Watoto Faraja Orphanage Centre, Mburahati, Dar es Salaam na kuahidi kuendelea kuheshimu misingi ya dini zote pamoja na kusaidia jamii ya watu wenye mahitaji maalumu.

Akikabidhi msaada huo, Mwakilishi wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dar es Salaam, Inderpreet Kaur Saini,amesema ni kuadhimisha kitendo cha watoto wanne wa Mtume wa 10 Singasinga, Guru Gobind Singh, kutolewa maisha yao kwa kutete msimamo wa imani yao.Ametaja msaada uliokabidhiwa kuwa ni vifaa vya shule, chakula, vinywaji, vifaa vya usafi, vifaa vya michezo na tauro za kike.

Inderpreet, amesema, Singasinga wanatambua umuhimu wa kusaidia jamii hususan ya watoto wenye mahitaji maalumu hivyo wamekuwa wakiwashirikisha vijana wao katika kuhudumia jamii watoto wenzao ili kuwa jenga kuwa nahuruma, moyo wa kutoa, kusaidia na kuyaishi maisha ya waasisi wa imani yao.

“Watoto wa kiume wanne wa Guru Gobind Singh Ji ni Baba Ajit Singh Ji, Baba Jujhar Singh Ji Baba Zorawar Singh Jin a Baba Fateh Singh Ji, ambao walitolewa maisha yao wakiwa wanapigana dhidi ya dhuruma wakiwa katika umri mdogo wa miaka tisa, saba, 14 na 16,”alisema.

Ameeleza imami ya Singasinga, inasimamia nguzo tatu ambazo ni kufanya swala, kufanya kazi yoyote halali halali na nguzo ya tatu ni kusaidia jamii hasa wasiyo kuwa nacho.Inderpreet ameeleza, wataendelea kuheshimu imani zingine kwa kutambua kuwa dini zote zinaabudu Mungu mmoja na wanadamu wote ni sawa na wana uhuru wa kuabudu kwa imani zao.

Katika hafla hiyo, Singasinga pia walikula chakula cha mchana na watoto wa kituo hicho.Akipokea msaada huo, mlezi wa watoto katika kituo hicho Karima Michael , ameishukuru jamii hiyo ya Singasinga kwa kuwakumbuka watoto wanao lelewa kituoni hapo na kuomba jamii kuiga mfano huo.“Singasinga wametuletea zawadi nyingi hapa.Watoto wamejisikia faraja kubwa na wamefurahi .

 Tunaomba jamii iige mfano huukuwatembelea watoto hawa,”ameeleza
Amesema kituo hicho kina watoto 91 kuanzia umri wa miezi saba hadi miaka 17, wa jinsi na dini zote.

Related Posts