TADB yatia saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) na mchongotv

Katika hatua ya kihistoria kwa sekta ya kilimo nchini Tanzania,Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania @tadbtz imeingia Mkatabawa Makubaliano (MoU) wa Miaka Mitano (5) na MchongoTelevisheni, kituo cha kwanza na pekee kinachojikita kwenyekutoa Habari za Kilimo,Uvuvi na Mifugo katika Ukanda wa AfrikaMashariki na Kati, ambapo kituo hicho kimewashwa rasmi kwamara ya kwanza kupitia kisimbuzi cha Startimes Chaneli namba134.

Ushirikiano kati ya TADB na Mchongo TV ni hatua muhimuinayolenga kukuza uelewa wa huduma za kifedha za kilimozinazotolewa na TADB, Pamoja na kuhamasisha wanawake, vijanana wadau wengine kuingia katika sekta ya kilimo kwa mtazamo wa kibiashara.

Related Posts