Dk. Biteko mgeni rasmi tamasha la Ijuka Omuka

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Ijuka Omuka litakalofanyika mkoani Kagera ambapo litazinduliwa Desemba 18,2024.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa leo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema tamasha hilo litazinduliwa litaanza dua kwa ajili ya kuuombea Mkoa Kagera, Taifa na kumuombea Rais wa Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema katika tamasha hilo kutakuwa na siku 10 za maonesho ya biashara yatakayofanyika katika viwanja vya CCM vilivyopo Manispaa ya Bukoba na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi.

Ameeleza kuwa tamasha la Ijuka Omuka ni la pili tangu kuanzishwa kwake mwaka jana na kusema na halikuweza kushirikisha watu wengi hivo mwaka huu wataweza kushiriki hasa wananchi wazawa wa mkoa huo.

“Wanakagera nitumie nafasi hii kuwakumbusha kuwa Ijuka Omuka ni neno la kihaya linalomaanisha kumbuka nyumbani na hivyo tumelenga wazawa wote kushiriki katika tamasha hili haijalishi wapo hapa Kagera au wapo nje ya nchi,na mwaka jana tulifanya Ijuka Omuka japo wachache wetu ndio tulishiriki ila hii ya mwaka huu itakuwa kiboko sana nawakaribisha wote kushiriki katika tamasha hilo,” amesema Hajjat Mwassa.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa katika hilo zitakuwepo tamaduni mbalimbali za kihaya ikiwemo burudani za kihaya,vyakula vya kihaya ikijumuishwa na mapishi tofauti tofauti yanayotokana na asili ya mkoa huo.

Amesema litasaidia kuwakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo na kupata nafasi ya kukaa na kujadili kwa pamoja ni kwa namna gani wataweza kushirikiana ili kuinua uchumi wa mkoa.

Aidha ,amewapa kipaumbele wananchi wa Mkoa Kagera kwa kuwepo matukio tofauti tofauti ndani ya siku nne ili kila mwananchi aweze kuburudika kwa manma yake ikiwemo muziki wa mirindimo ya Pwani.

Related Posts

en English sw Swahili