-Akabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya mamilioni ya fedha katika Jimbo la Chwaka
MWAKILISHI wa Jimbo la Chwaka visiwani Zanzibar ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu((NEC) Oganaizesheni Issa Gavu amesema Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi imefanya maendeleo makubwa kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu.
Sambamba na hayo amesema wananchi wa Jimbo la Chwaka wameendelea kushuhudia changamoto mbalimbali zikipatiwa ufumbuzi pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya barabara,elimu,afya na maji huku akielezea wazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndicho kilichokuwa na uthubutu na utayari wa kuwatumikia wananchi.
Gavu ameyasema hayo leo Desemba 14,2024 alipokuwa akielezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo la Chwaka ambapo pia amekabidhi pikipiki 20 zenye thamani ya Sh.milioni 72 , Vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh.milioni 17.
Pia amekabidhi vitenge ,fulana na kofia vyenye thamani ya Sh.milioni 14 , michango kwa jamii milioni 22,vyarahani 100 thamani ya Sh.milioni 30,bati,saruji na vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh.milioni Saba pamoja na mashine 15 za kuprintia ambapo kila Moja thamani ni zaidi ya Sh.milioni 2.1.
Akieleza zaidi amesema hana shaka katika uchaguzi ujao viongozi kuanzia diwani, Mbunge na Mwakilishi pamoja na Rais watatoka Chama Cha Mapinduzi huku akifafanua kuna vyama 19 lakini hakuna chama, jumuiya wala taasisi yenye utayari na uthubutu wa kuweza kuliongoza Taifa letu kwa mfanisi na mafanikio makubwa kama wanayoyaona kwa Chama Cha Mapinduzi.
“Sisi watu wa Chwaka ni mashahidi na ni mashuhuda kwenye serikali hii ya Awamu ya nane yako mambo yalikuwa yanatukwaza , Serikali hii ya CCM chini ya uongozi wa Dk.Hussein Ali Mwinyi tumepiga hatua kubwa sana katika maendeleo ndani ya watu wa Jimbo la Chwaka
“Yapo maeneo tulikuwa na changamoto za maji , elimu ,afya sambamba na miundombinu lakini leo hii jitihada na mipango ya Serikali kila mmoja wetu anaiona kama haijakamilika basi iko kwenye mchakato,kama haiko katika mchakato iko katika mfumo wa kutafuta utaratibu mzuri wa kufanikisha kuondoa changamoto hizo.
“Tunayo miradi ya kitega uchumi kwa ajili ya kuwezesha wajasiriamali, tunavyo vyuo vya ufundi pamoja na vituo vya elimu,hayo yote ni matunda ya kukichagua Chama Cha Mapinduzi.Ninachokuombeni watakapokuja wenzetu kuja kuzungumza nanyi msiwakasirikie wala msigombane nao.
“Sisi hoja yetu tutakwenda kuijibu kwa vitendo lakini tunawajibu wa kujiandaa vizuri na utakapofika wakati wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura Jimbo letu liwe na malengo ya kufikia ufanisi kwa asilimia 100 katika uboreshaji wa daftari la kupiga kura,”ameelezea Gavu.
MWAKILISHI wa Jimbo la Chwaka visiwani Zanzibar ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu((NEC) Oganaizesheni Issa Gavu,akikabidhi pikipiki 15 zenye thamani ya Sh.milioni 72 , Vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh.milioni 17. leo Desemba 14,2024 alipokuwa akielezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu katika Jimbo la Chwaka.
MWAKILISHI wa Jimbo la Chwaka visiwani
Zanzibar ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu((NEC) Oganaizesheni
Issa Gavu, Akizungumza leo Desemba
14,2024 alipokuwa akielezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu katika
Jimbo la Chwaka ambapo pia amekabidhi pikipiki 15 zenye thamani ya
Sh.milioni 72 , Vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh.milioni 17.