PROGRAMU YA ‘CODE LIKE A GIRL’ IMEWAJENGEA UWEZO WA TEHAMA WASICHANA MKOANI DODOMA

 Jumla
ya wanafunzi wa kike 2600 wamejengewa uwezo wa masomo ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Kampuni ya simu ya Mikononi ya
Vodacom Tanzania tangu 2018 mpaka mwaka huu kupitia program ya Code Like
a Girl

Mkuu wa Kanda ya kati wa Vodacom Tanzani, Joseph Sayi
alisema hayo leo desemba 13 wakati alipokuwa akifunga mafunzo hayo ya
TEHAMA yaliyofanyika Chuo kikuu cha Dodoma (Udom).

Alibainisha
kuwa mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa kwa awamu kwa baadhi ya Mikoa
hapa nchini yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa masomo ya Sayansi,
Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) wanafunzi hao wa kike kwa
ufadhili wa Vodacom Tanzania PLC.

 Meneja
wa Kampuni ya  Vodacom Tanzania Kanda ya Kati Joseph Sayi (kushoto)
akimkabdhi cheti mwanafunzi Winnie Futa wakati wa kufunga mafunzo ya
kuwajengea uwezo  wanafunzi wa kike katika masomo ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofadhiliwa na Vodacom.

Meneja
wa Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania Kanda ya Kati ,Joseph Sayi
(kulia) akizungumza na wanafunzi wasichana  kutoka Kanda hiyo wakati wa
kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo katika masomo ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Udom Jijini
Dodoma jana kwa ufadhili wa Vodacom.

Meneja
wa Kampuni ya  Vodacom Tanzania Kanda ya Kati Joseph Sayi (kushoto)
akimkabidhi  begi  mwanafunzi Emmeline Kitali wakati wa kufunga mafunzo
ya kuwajengea wanafunzi wa kike uwezo  wanafunzi wa kike katika masomo
ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)  yaliyofanyika Chuo
kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhiliwa na Vodacom. 

Baadhi
ya wanafunzi wa kike kutoka shule za sekondari Kanda ya kati
wakijifunza jinsi ya kutumia kopyuta kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo
katika masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA )
yaliyofanyika Chuo kikuu cha Udom Jijini Dodoma jana kwa ufadhili wa
kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom Tanzania.

Related Posts