Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limesaini mkataba na Ushirika wa Maisha Gemu ya Zanzibar ili kuwa wakala wa nishati safi na salama ya Rafiki Briquette visiwani humo.
Amesema, STAMICO imechukua hatua madhubuti za kuhakikisha inashiriki kikamilifu katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa nishati safi huko Zanzibar
Amesema, mkataba huu unathibitisha dhamira ya makusudi ya ya STAMICO katika kuhakikisha mkaa huu unapatika nchi nzima ili kushiriki kikamilifu ajenda ya Serikali ya kuhamasisha
matumizi ya nishati Safi ya kupikia na kufikia lengo la taifa la kutunza mazigira.
“Niwashukuru sana ushirika wa Maisha Gemu kwa kuibeba ajenda ya matumizi ya Nishati safi katika kurunza mazingira na kuwa vinara wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi huko zanzibar” alisema Bw.Magala.
Ameongeza kuwa STAMICO imendelea kuongeza Viwanda vya uzalishaji kwa mikoa mingine miwili ikiwemo Dodoma na Tabora hivyo kufanya jumla mitambo mikubwa ya uzalishaji kufikia minne.
Naye, Mwenyekiti wa Ushirika wa Maisha Gemu Bw. Alawi Idarous ameshukuru hatua hii ya utiaji sahihi wa mkataba na kuahidi kushiriki na kufuata taratibu zote zilizomo katika mkataba
Ameishukuru STAMICO kwa kupeleka elimu ya Rafiki Briquettes Visiwani Zanzibar jambo lililowafungulia fursa ya kibiashara sambamba na kutoa hamsa ya kushiriki kwenye masuala ya utunzaji wa mazingira kupitia nishati ya Rafiki Briquettes
Amesema, mkaa huu unatarajia kuleta matokeo chanya kwa upande wa Zanzibar kwa kupunguza changamoto ya upatikanaji wa nishati safi ya kupikia sambamba na kutunza mazingira.
STAMICO imeendelea kufungua fursa za kibiashara kwa vikundi mbalimbali ili kuweza kuwa mawakala na wasambazaji wa nishati hiyo na kushiriki kikamilifu.