Mamlaka ya Mapato Tanzania Tra Mkoa wa Iringa Imeendelea kudumisha mahusiano Mazuri na kuwashukuru wafanyabiashara wake Mkoani hapa kwa kuendelea kutimiza wajibu wake wa kulipa Kodi kwa wakati
Hii ni mara baada ya Meneja wa Mamlaka ya mapato Tanzania Tra Mkoa wa Iringa Bw. Peter Jackson akiwa pia ameambatana na meneja msaidizi Bw. Gwamaka Pholld walipowatembelea walipaKodi Ndg Rajan Marwaha Ambaye ni Mkurugenzi wa SAI VILLA HOTEL na mlipa kodi Ndg Baptista Filipatali Ambaye ni mkurugenzi wa Iringa Suset Hotel lengo kuwashukuru kwa kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi
Meneja wa Tra Mkoa wa Iringa amesema ni muhimu kutii wajibu wa kulipa kodi kwani taifa lolote ikiwemo pia la Tanzania kwasababu linaendeshwa kwa shughuli za fedha zitokanazo na kodi .