TRA mkoa wa Iringa yazidi kudumisha mahusiano na wafanyabiashara

Leo tarehe 14 Disemba Mamlaka ya Mapato Tanzania Tra Mkoa wa Iringa Imeendelea kudumisha mahusiano Mazuri na wafanyabiashara wake Mkoani hapa na hii ni mara baada ya Meneja wa Tra Mkoa wa Iringa Bw. Peter Jackson wakiwa wameambatana na Meneja Msaidizi wa ukaguzi na Ufuatiliaji wa Madeni Bw. Gwamaka Pholld kuzungumza na viongozi wa Chemba ya wafanyabiashara TCCIA

Akizungumza na viongozi wa chemba ya wafanyabiashara TCCIA mkoani Iringa meneja wa Tra amewashukuru kwa niaba ya wanachama wao kwa kutimiza wajibu wa kulipa Kodi

Pia chemba hiyo pamoja na Tra mkoani hapo wamekubaliana kwa pamoja kwamba TCCIA mkoa wahamsishe wanachama wao wafanye malipo ya awamu ya nne 2024 mapema na kuwasilisha ritani za VAT mapema

Related Posts