Vodacom Tanzania Kuboresha Huduma kwa Kuunganisha My Vodacom App na M-Pesa Supa App

 

Vodacom Tanzania inayo furaha kutangaza kuunganishwa kwa My Vodacom App na
M-Pesa Supa App, hatua inayolenga kurahisisha na kuboresha zaidi huduma kwa
wateja.

Kupitia muunganiko huu, wateja
wataweza kufurahia huduma zote wanazozipenda za Vodacom kwenye aplikesheni
moja, hivyo kuongeza ufanisi na urahisi wa matumizi.

Kama sehemu ya mabadiliko haya,
My Vodacom App itasitishwa rasmi tarehe 1 Desemba 2024. Tunawahimiza wateja
wote kupakua na ku-update M-Pesa Supa App ili kuendelea kufurahia huduma zetu
bila usumbufu.

Hatua hii inadhihirisha dhamira
yetu ya kuboresha huduma kwa wateja kupitia suluhisho za kibunifu.

Asante kwa kuichagua Vodacom
Tanzania.

Related Posts