Mastercard Foundation EdTech Fellowship kuwezesha Kampuni za Elimu na Teknolojia

Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv

KAMPUNI ya Sahara Consult, kwa kushirikiana na Mastercard Foundation imetoa wito kwa wajasiriamali chipukizi wanaotumia teknolojia kutengeneza suluhisho kwenye elimu kutuma maombi yao kwenye awamu ya pili ya mradi wa ‘Mastercard Foundation EdTech Fellowship’. Nchini

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mtendaji Mkuu wa Sahara Consult, Jumanne Mtambalike wakati wa shughuli ya ‘Demo Day’ ambapo washiriki 10 wa awamu ya kwanza ya mradi wa Mastercard Foundation EdTech Fellowship walipata nafasi ya kuwasilisha suluhisho zao zinazotatua changamoto mbalimbali za elimu.

Mradi huo ambao umetengenezwa kuwezesha kampuni changa zinazojihusisha na teknolojia na elimu barani Afrika, unatekelezwa kwa kushirikiana na vituo vya ubunifu pamoja na wadau wanaojikita kwenye kukuza kampuni changa za teknolojia na elimu,.

Amesema mradi huo unatoa fursa ya mafunzo ya kibiashara na ufadhili wa kifedha pamoja ujuzi juu ya nadharia ya science ya kujifunza, huku ukiwaandaa kukuza biashara zao kuwa uendelevu na zenye kuleta matokeo chanya.

Imeelezwa kuwa, kupitia awamu ya pili ya mradi huo, kampuni changa za teknolojia na elimu ambazo ziko kwenye hatua ya ukuaji na zilizobuni suluhisho zinazotatua changamoto za elimu Tanzania zitachaguliwa.

Ameongeza kuwa, washindi wa awamu ya kwanza ya mradi walichaguliwa mwaka 2024 na walifanya mafunzo ya miezi 6 ambapo waliweza kuwasilisha suluhisho zao za elimu za kibunifu kwa wawekezaji, wadau wa serikali, watoa elimu, wanafunzi na wadau wa maendeleo, ikiwa ni namna ya kutafuta fursa ya kuwezesha suluhisho zao kutumiwa nchini ili kupata matokeo chanya kwenye maswala ya elimu.

Suluhisho hizo ni pamoja na mikebe ya vifaa vya masomo ya sayansi, majukwaa ya kujifunza mtandaoni pasipo kutumia mtandao, pamoja na mifumo ya kusimamia uendeshaji shule. Kwa kipindi cha mwaka 2024 cha utekelezaji wa mradi, kampuni changa kumi za kitanzania ambazo ni; Taifa Tek, MITzKITS, Kilimanjaro Planetarium, Smartdarasa, Shule Yetu, Smartcore, ShuleSoft, Fiqra Academy, Infotaaluma na na Mtabe kwa pamoja zilifanikiwa kufikia wanafunzi 50,000.

Akizungumza siku ya ‘Demo Day’ Mtendaji Mkuu wa Sahara Consult, Jumanne Mtambalike amesema, “kwenye nyakati hizi, ni muhimu kujumuisha teknolojia za kisasa na ubunifu kwenye mifumo yetu ya elimu, kama tuna shauku ya kutatua baadhi ya changamoto kwenye mfumo wetu wa elimu.

“Kampuni hizi chipukizi zilizojikita kutatua changamoto za elimu, zimeweza kutumia nguvu ya teknolojia kuboresha elimu hivyo tunapotoa wito wa kutuma maombi ya kushiriki kwenye awamu ya pili ya mradi huu, nahimiza vijana kwenye sekta ya ubunifu na teknolojia na wenye shauku ya kuletea matokeo chanya, kutuma maombi yao.”

Related Posts