Polisi Iringa yawasaka askari wanaotuhumiwa kwa mauaji

Iringa. Polisi Mkoa wa Iringa inawasaka askari namba F.4987 Sajenti Rogers wa Kituo cha Polisi Ipogolo na askari wa Jeshi la Akiba (Mgambo) Thomas Mkembela kwa tuhuma za mauaji ya Nashon Kiyeyeu (23), mkazi wa Mtaa wa Nyamhanga, Manispaa ya Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili, Desemba 15, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema inadaiwa kuwa Desemba 14, 2024  Sajenti Rogers alipokea taarifa kutoka kwa mwananchi (hakumtaja jina) kuwa anamtuhumu Kiyeyeu kuwa amemwibia simu.

Amesema baada ya askari huyo kupokea taarifa kwa kushirikiana na mgambo walimkamata mtuhumiwa, ikidaiwa walimpiga hali iliyosababisha apoteze fahamu.

Askri wa Jeshi la Polisi, Sajent Rogers Mmari ambaye anatafutwa kwa tuhuma za mauaji.

“Baada ya kumpiga na kuona amepoteza fahamu walimpeleka hospitali moja binafsi na baadaye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na ikabainika kuwa ameshafariki dunia, walitoweka na kukimbilia kusikojulikana,” amesema.

Kamanda Bukumbi ametoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zaidi kuhusu watuhumiwa wazisisite kutoa ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.

Related Posts