DKT. YONAZI AMPONGEZA MHE. BALOZI MUTATEMBWA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt, Jim Yonazi akiwa katika picha ya pamoja wakati wa kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu Dkt Henry James Kilabuko na Kumuga Mhe. Balozi Anderson Mutatembwa tukio lilofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome Jijini Dodoma.

Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) wakiwa katika matukio tofauti wakati wa kumkaribisha Naibu Katibu Mkuu Dkt Henry James Kilabuko na Kumuaga Mhe. Balozi Anderson Mutatembwa tukio lilofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Ngome Jijini Dodoma.

Na. Mwandishi Wetu – Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt Jim Yonazi amempongeza Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bw. Anderson Mutatembwa kwa Kuteuliwa kuwa Balozi.

Dkt. Yonazi Ametoa pongezi hizo Tarehe 16 Disemba 2024, wakati akimuaga Mhe. Balozi Mutatembwa na Kumakaribisha Naibu katibu Mkuu mpya Dkt. James Kilabuko.

Dkt. Yonazi amempongeza Balozi Mutatembwa kwa kufanya kazi ya ushauri kwa utulivu aliyotokana hekima aliyojijengea na kujaliwaa na Mwenyezi Mungu kuwa nayo “Na ndiyo maana Mhe. Rais ameweza kukuamini na kukuteuwa katika nafasi ya Ubalozi ili uweze kumuwakilisha yeye pamoja na Nchi katika maeneo ambayo atakayoona inampendeza.” Alifafanua

Aliendelea kusema kuwa, nafasi ya ubalozi ni nafasi nyeti na adhimu sana na ni fursa inayopatikana kwa watu wachache sana, “umepata fursa nyeti sana ya kuitumikia Taifa naamini utaendelea kufanya kazi kama ambavyo umekuwa ukifanya hapa na utakaoenda kufanya nao kazi watafaidika na kufurahia kama tulivyo faidika sisi.” Alibainisha Dkt. Yonazi

Akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu mpya Dkt. James Kilabuko, Katibu Mkuu Dkt. Yonazi alisema Ofisi ya Waziri Mkuu ni Ofisi yenye majukumu mazito yenye watumishi wachapakazi wenye kutizama tija katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku.

Naibu Katibu Mkuu, Dkt. James Kilabuko Alimshukuru Mhe. Rais kwa kumteuwa katika nafasi hiyo na kuona kwamba anaweza kumsaidia Katibu Mkuu Kiongozi katika nafasi hiyo, aliendea kusema kuwa anategemea kupata ushirikiano kutoka kwa Watumishi na Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika kumsaidia Katibu Mkuu Dkt. Jonazi kiutendaji na kufikia malengo yanayotegemewa na mamlaka za juu.

Kwa Upande wake Mhe. Balozi Anderson Mutatembwa , alimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea Kumuamini na kumteuwa katika nafasi hiyo.

Aidha, Ameishukuru Menejimenet ya Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu pamoja na watumishi wa Ofisi hiyo kwa ushirikiano waliomupatia wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ofisini hapo, aliendelea kusema kuwa ni sehemu ambayo atapakumbuka kwani amefanya kazi kwa amani na Utulivu wa hali ya juu.

Related Posts