Maisha ya mshambuliaji Joseph Guede ndani ya klabu ya Singida Black Stars yamefikia baada ya kutupiwa virago.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga klabu yake imetangaza usiku huu kuwa imeachana naye baada ya kudumu kwa miezi mitano pekee.
Guede hakuwa na miezi mitano mizuri ndani ya Singida baada ya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara huku akiwa pia hajafunga bao lolote mpaka Leo anaachwa.
Kabla ya hapo akiwa Yanga ndani ya miezi sita aliifungia timu hiyo mabao 10 kwenye mashindano yote aliyocheza lakini Mabingwa hao wa soka wakagoma kumuongezea mkataba.
Singida inarudi sokoni kutafuta mshambuliaji mwingine mwenye makali ambaye atakuja kusaidiana na mshambuliaji wao kinara wa ufungaji kwenye ligi na klabu hiyo Elvis Rupia mwenye mabao saba.
Guede anakuwa mchezaji wa kwanza kuachwa na Singida msimu huu huku akitanguliwa na kipa Mohammed Kamara aliyetimkia Pamba na kiungo Najim Mussa aliyepelekwa Namungo wawili hao wakitolewa kwa mkopo wa miezi sita kila mmoja.