KenGold yaanza na wanne dirisha dogo

WAKATI KenGold ikianza kusuka kikosi chake kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo, timu hiyo inakabiliwa na ratiba ngumu katika michezo mitano kupambania nafasi ya kubaki Ligi Kuu.

Tayari dirisha dogo limefunguliwa Desemba 15 mwaka huu, ambapo vijana hao wa wilayani Chunya, wamevuta sura mpya nne kwa ajili ya kuongeza nguvu na kupambana kukwepa janga la kushuka daraja.

Habari ilizopata Mwanaspoti ni kuwa, tayari wachimba dhahabu hao wamewavuta Sadala Lipangile aliyekuwa Biashara United inayoshiriki Ligi ya Championship. Wengine ni Abdalah Nassir (Miembeni), Mathias Juviliani (KVZ) zote za Zanzibar na Sambale Komanje kutoka

Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza, haijawa na matokeo mazuri ikiburuza mkia kwa pointi sita baada ya michezo 14.

Hadi sasa timu hiyo imebakiwa na mechi moja dhidi ya Simba ugenini itakayopigwa kesho Jumatano ili kukamilisha mzunguko wa kwanza.

Baada ya kucheza na Simba, timu hiyo itabaki ugenini kucheza dhidi ya Singida Black Stars na Yanga, kisha kurudi nyumbani Mbeya kukabiliana na Fountain Gate, kisha itawafuata Tabora United.

Mechi hizo KenGold inakwenda kukutana na timu zenye ushindani mkali na zote zikiwa nafasi tano za juu, hali inayoipa mtihani mzito kwenye kukwepa kushuka daraja.

Kocha Mkuu wa KenGold, Omary Kapilima alisema watafanya mabadiliko kikosini humo kuhakikisha wanabaki salama Ligi Kuu.

Related Posts