Mpango Awataka Viongozi kuwa Mstari wa mbele Mapambano Dhidi ya Rushwa.

 

 

Na Jane Edward,Arusha

Makamo wa Rais Dkt Philip Mpango amewataka viongozi wote nchini kuwa mstari wa mbele katika kuongoza mapambano dhidi ya  vitendo vya rushwa kwani viongozi wanaposhindwa kutimiza wajibu wao vitendo vya rushwa vinaendelea kushamiri na kuwafanya waanchi kukosa Imani na serikali yao.

Mpango ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka 2024 wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa [TAKUKURU]unaofanyika Mkoani Arusha kwa siku nne.

 Amesema kuwa vitendo vya rushwa vinarudisha nyuma maendeleo kwa upotevu wa rasilimali za umma na kurudisha nyuma jitihada za maendeleo na kwamba uadilifu wa viongozi na watumishi wa umma ni sharti muhimu katika mapambano hayo ambapo kiongozi anatakiwa kuwa mtu ambaye hapaswi kutiliwa shaka

Aidha mpango amesema anaunga mkono kauli mbiu isemayo ‘’kuzuiya rushwa ni jukumu lako na langu;tutimize wajibu wetu’’  ambapo amesema dhamira ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuzuia rushwa kwa nguvu zote katika maeneo ya uwaibikaji ili nchi za Afrika ziige mifano kutoka kwetu na sio kuonekana sio sehemu salama kwa kukithiri kwa vitendo hivyo.

 Naye mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Crispin Chalamila amesema Taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya rushwa na kuhamasisha ushiriki mapambano dhidi ya adui rushwa sannjari na uelimishaji kwa makundi mbaimbali katika jamii kuanzia vijijinu hadi mijini kupitia  mikutano,midahalo,minada,warsha Pamoja na semina mbalimbali.

 Chalamila ameendelea kusema kuwa wanajivunia uendeshaji wa kesi dhidi ya vitendo vya  rushwa ambapo Jamhuri imeshinda kesi kwa asilimia 75.9 tofauti na mwaka jana ambapo Jamhuri ilishinda kesi kwa asilimia 67.7katika kesi zilizotolewa maamuzi,na kwamba bado safari  ndefu  kufikia wastani wa juu Zaidi ambapo mkutano huo utaleta majawabu kamili.

 Aidha amemuhakikishia Makamo wa Rais kuwa kupitia mkutano huo wamejipanga kuhakikisha wanatafakari na kuja na majibu ya Pamoja kudumisha TAKUKURU ili kukidhi matamanio ya Watanzania  katika mapambano dhidi ya Rushwa.

 

Related Posts