DODOMA, 13 DISEMBA 2024 – Jumla ya wanafunzi wa kike 2600 wamejengewa uwezo wa masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Kampuni ya simu ya Mikononi ya Vodacom Tanzania tangu 2018 mpaka mwaka huu kupitia program ya Code Like a Girl Mkuu wa Kanda ya kati wa Vodacom Tanzani, Joseph Sayi alisema hayo leo desemba 13 wakati alipokuwa akifunga mafunzo hayo ya TEHAMA yaliyofanyika Chuo kikuu cha Dodoma (Udom). Alibainisha kuwa mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa kwa awamu kwa baadhi ya Mikoa hapa nchini yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) wanafunzi hao wa kike kwa ufadhili wa Vodacom Tanzania PLC.