DB Lioness yaivua ubingwa Vijana Queens

DB Lioness imetwaa ubingwa wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL),  baada ya kuifunga Vijana Queens katika michezo 3-2.

Vijana iliyokuwa bingwa mtetezi wa ligi hiyo, ilipoteza pia kombe la ligi ya taifa ya kikapu NBL mwaka huu.

Fainali hiyo  ilishuhudiwa na watazamaji wengi kwenye Uwanja wa Donbosco Upanga.

Katika mchezo wa kwanza wa fainali hiyo, Vijana ilishinda kwa pointi 57-36, mchezo wa pili ikashinda tena kwa pointi 62-48.

Fainali ya tatu DB Lioness ikashinda kwa pointi 61-54 na ya nne Lioness ikapata ushindi wa chee, baada Vijana kutotokea uwanjani.

Kocha wa Vijana, Bahati Mgunda alisema walishindwa kwenda uwanjani   kutokana na wachezaji wake kusafiri kwenda mkoani Kilimanjaro kwenye mashindano ya Shimivuta.

“Katika fainali ya tano, tulipeleka timu uwanjani baada ya wachezaji wangu kuwasili mchana, baada ya fainali kumalizika walipanda  basi na kurudi  Kilimanjaro.

Katika mchezo huo, DB Lioness iliongoza kwa pointi 18-15 na 20-10, hadi kufikia mapumziko washindi walikuwa wanaongoza kwa pointi 38-25.

Robo ya tatu Vijana ilifunga pointi 19-13 na ya nne ikapata pointi 14-13.

Katika mchezo huo, Taudencia Katumbi wa DB Lioness alifunga pointi 17, na upande wa Vijana  Noela Renatus alifunga pointi 14.

Related Posts