Sativa amlipia Lissu fomu ya kugombea Uenyekiti Chadema

 

TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema kuwa Fomu ya kugombea uenyekiti wa Chama hicho imelipwa na Sativa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Hizi fomu zinatakiwa zilipiwe hiyo ada yake shilingi 1,500,000 nilitaka nilipe mimi mwenyewe Kuna wanachama wema wanaofikiri kama mimi uchaguzi huu uwe mwanzo mpya wa chama chetu ambao wamechanga fedha kwa ajili ya kulipia hii gharama ya kuchukulia fomu.

“Lakini hata hivyo hiyo fadha waliochanga wanachama haitatumika kulipia hiyo fomu na fedha yangu haitatumika hiyo shillingi 1,500,000 imetolewa na mwanachama wetu mmoja anayeitwa Edger Edson Mwakabela jina maarufu Sativa,” amesema Lissu na kuongeza.

“Sativa ndiye aliyekamatwana kuteswa na watu wa usalama na kuteswa mungu si Athumani Sativa yuko hai leo yuko uhamishoni imebidi akimbie Tanzania ili wasimuue.”

Lissu alisema: “Amenipigia simu ameniambia naomba nikulipie hiyo fomu kwa sababu naamini kama ukiwa Mwenyekiti wa chama utafanya kazi inayohitaji nchi hii ya kupigania haki za Watanzania kupigania Tanzania mpya itakayohakikisha kwamba hatutekwi na kupotezwa kama Soko, Bensaanane, Azori Gwada, Simon Kangunye.

“Akasema nakulipia hiyo fomu kwa sababu naamini ukiwa mwenyekiti utaongoza mapambano ya kudai haki ili isije kutokea watu kutekwa na kuteswa kama nilivyoumizwa mimi hayo ndio maneno aliyoniambia Sativa jana wakati ananiambia atanilipia fomu”

Amesema kuwa akiwa Mwenyekiti atahakikisha watu wanaotenda haki ndio watakaoshika mamlaka.

About The Author

Related Posts