TASAC yafanya ukaguzi Meli ya Azam.

 

Na Chalila Kibuda ,Michuzi Tv

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa linaendelea na ukaguzi vyombo vya usafirishaji  majini kutokana na baadhi vyombo hivyo kuzidisha abiria au mizigo katika Siku kuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza katika ukaguzi wa Meli ya Azam Afisa Mkaguzi Mkuu wa Shirika hilo Rashid Katonga uliofanyika Bandarini jijini Dar es Salaam.

Katonga amesema kuwa katikq kipindi hiki kumekuwa na baadhi ya vyombo vya usafirishaji  majini kuongeza  idadi ya abiria au mizigo kutokana na kuwepo kwa uhitaji wa watu wengi kufanya safari au kusafirisha mizigo.

Amesema  katika kipindi hiki TASAC imejipanga kufanya  ukaguzi kwa kuangalia uwezo wa chombo na abiria wanaotakiwa na wakibaini safari inasitishwa pamoja kulipa gharama za ukiukaji wa sheria.

Aidha Amesema  kuwa ukaguzi huo unakwenda pamoja na kutoa elimu kwa abiria katika kuwakumbusha wajibu wa kusafiri kwa kutumia vyombo hivyo.

Nahodha wa Azam Marine Ferouz Kassim amesema kuwa wanafuata matakwa ya sheria katika kutoa huduma za usafiri majini.

Kassim amesema kuwa TASAC kufanya ukaguzi ni jambo zuri kutokana kukumbusha wasafirishaji kuelewa wajibu katika vipindi vyote katika kulinda maisha ya wasafiri.

 

Related Posts