WAZIRI
wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa ameiagiza
Bodi ya Shirika La Mawasiliano Tanzania (TTCL) kuhakikisha linasimamia
vyema shirika hilo na kuhakikisha liendeshwa kibiashara.
Maagizo
hayo ameyatoa leo Desemba 16, 2024 Jijini Dar es Salaam, wakati
akizindua Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).
Mhe.
Silaa amemtaka Mwenyekiti wa Bodi hiyo David Nchimbi kutengeneza
mpango utakalitoa Shirika lilipo na kulipeleka kwenye uendeshaji
kibiashara ikiwa ni kutekeleza maagizonya Rais Samia,
“Rais
Samia Suluhu Hassan alielekeza shirika kuhakikisha linaendeshwa
kibiashara hivyo Mwenyekiti atengeneze mpango utakaotutoa tulipo na
kupeleka shirika kwenye uendeshaji kibiashara ” amesema Mhe. Silaa.
Aidha
Mhe. Silaa amesema serikali imewekeza fedha nyingi kwenye miundombinu
ya mawasiliano ya Taifa ikiwemo mkongo wa taifa ambao umeunganisha
karibu nchi nzima na kuna miradi mbalimbali na kuna kuna miradi
mikubwa ya mawasiliano mradi wa ktuo cha Taifa cha data hivyo ni nia ya
Rais Samia kuona uwekezaji huo mkubwa uliofanywa kwa fedha za
wananchi uweze kuleta tija kwa kujiendesha kibiashara na kuiona ile
thamani ya fedha iliyotolewa.
Amesema iwapo Shirika likiendeshwa vyema linaweza kukuza sekta mbalimbali na kuleta mapinduzi makubwa ikwenye uchumi wa nchi.
“Hivyo
Mwenyekiti na wajumbe tekelezani hayo na ninawaahidi milango ya
wizara iko wazi, na mtambue uendeshaji wa shirika uko chini ya bodi
hivyo uwajibikaji uko chini ya mabega yenu siimamieni menejimenti
vizuri ili tufike tuendako” amesema,
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa bodi hiyo Nchimbi ameshukuru Rais Samia
Suluhu Hassan kumteua katika nafasi hiyo na kuahidi kuwa na shirika
jipya na kulipeleka mbele zaidi na kwa kasi.
Amesema wajumbe wana uwezo mkubwa na wamesikia maelekezo yaliyotolewa na watayafanyia kazi na hakuna litakalowashinda .