Na Janeth Raphael MichuziTv
Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, amekemea tabia ya baadhi ya Watumishi wa Umma kukaimisha nafasi kwa watu wasio na sifa, huku akisema kwamba jambo hili husababisha migogoro ndani ya Taasisi na hupelekea watumishi waliokaimu nafasi kutopewa haki zao.
Waziri Simbachawene amewasihi viongozi wa Taasisi kuhakikisha kuwa wanateua watu wenye sifa kwa nafasi za kazi ili kuepuka migogoro na upotevu wa haki.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo mapema Leo hii Desemba 17,2024 Jijini Dodoma wakati akifungua Kikao kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
Na kuwataka wote wanaojihusisha na tabia hizo kuacha mara moja na Taasisi ambazo Watumishi wake wamaebainika kuwa na mapungufu yaliyoanishwa mamlaka ya nidhamu ya watumishi katika Taasisi hizo ichukue hatua stahiki dhidi ya watumishi hao kwa majibu wa taratibu za Utumishi wa Umma.
“Napenda pia nizungumzie kidogo kuhusu kukaimu nafasi,kinachoendelea katika maeneo yenu wakati mwingine mnakaimisha mtu ambye hata iweje hata thibitishwa kwa cheo hicho,mnatengeneza vita katika taasisi zenu. Unapokaimisha mtu kaimisha mtu ambaye anasifa kwasababu kukaimishwa kuna haki zake pia, hivyo mtu ukimakaimisha kama hana sifa hana haki ya kuzipata hizo haki, lakini pili hata thibitishwa katika cheo hicho, hili tuliacheni katika Taasisi yako lama yupo mwenye sifa hata kama humpendi mpe nafasi kwani Taasisi sio yako wala sio mali yako ni mali ya wote”.
” Hivyo, nitoe wito kwa wote wanaojihusisha na tabia hiyo kuacha mara moja. Aidha, Taasisi ambazo watumishi wake wamebainika kuwa na mapungufu yaliyoainishwa, Mamlaka ya Nidhamu ya watumishi katika Taasisi hizo ichukue hatua stahiki dhidi ya watumishi hao kwa mujibu wa taratibu za Utumishi wa Umma na ningependa kupata taarifa kuhusu namna walivyoshughulikia masuala hayo na kuyahitimisha”.
Aidha Waziri huyo ameongeza kuwa Serikali inatambua wajibu wa watumishi wa Umma unaendana na haki zao,hivyo Serikali kupitia ofisi hiyo kwa mwaka 2023/2024 imewapandisha vyeo watumishi 229,159,kuwabadilisha kada Watumishi 9,654 na kutoa nyongeza ya mshahara wa mwaka Watumishi wake na kutoa vibali vya ajira kwa kada mbalimbali.
“Ninatambua kuwa wajibu wa Watumishi wa Umma unaendana na haki zao. kwa kutambua hilo, katika bajeti ya mwaka 2023/2024 Serikali kupitia Ofisi hii imewapandisha vyeo watumishi 229,159 na kuwabadilisha Kada Watumishi 9,654. Vilevile, Serikali imetoa nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa watumishi wake na itaendelea kuboresha maslahi ya watumishi kulingana na uwezo wa uchumi. Ni jukumu lenu kama wasimamizi wa watumishi wa Umma kuendelea kuwasimamia watumishi walio chini yenu kwa kuwaelimisha kuhusu haki na wajibu wao ili wanapodai haki wajue kuwa kuna wajibu wanapaswa kuwa wametekeleza”.
“Serikali kwa kutambua kuwa Rasilimaliwatu ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa imekuwa ikitoa vibali vya Ajira kwa Kada mbalimbali. Katika mwaka wa Fedha 2024/2025 Serikali imetoa kibali cha kuajiri watumishi arobaini na tano elfu na themanini (45,080) wa kada mbalimbali, kati yake watumishi elfu kumi mia tatu tisini na sita (10,396) ni wa Kada za Afya, watumishi elfu kumi mia tano tisini (10,590) wa kada za Ualimu na Watumishi elfu ishirini na nne na tisini na nne (24,094) wa Kada nyingine.
Aidha, nimetaarifa kuwa mchakato wa ajira wa watumishi wa kada za Afya umekamilishwa na watumishi hao tayari wameshapangiwa vituo vya kazi. Niwatake waajiri kuhakikisha wanawapatia mafunzo ya awali, kuwalipa stahiki zao na wanawajengea uwezo. Vilevile, ni wajibu wa Waajiri wote kutenga bajeti kwa ajili ya Ajira mpya kulingana na mahitaji halisi ya Taasisi zao”.
“Pia Katika kutekeleza dhana ya uwazi na uwajibikaji Ofisi ninayoiongoza imeweka Mifumo ya uwazi na uwajibikaji kupitia “Sema na waziri utumishi” na e-Mrejesho ili kupokea mrejesho wa watumishi na wananchi kwa ujumla. Aidha, kwa sasa Ofisi inaendelea na usanifu wa Daftari la Kielekroniki la Huduma za Serikali (Government Service Directory) ambalo baada ya kukamilika kwake itawezesha wananchi na watumishi kufahamu huduma zinazotolewa na Taasisi za Umma, gharama kama zipo na michakato ya kufuatwa katika kupata huduma hizo. Uwepo wa Daftari hilo utasaidia kudhibiti Vishoka wanaoingilia huduma zinazotolewa na Serikali kwa sababu huduma zote zinazotolewa na Serikali zitakuwa wazi”.
Awali akizungumza Naibu Waziri Ofisi wa Raisi,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bwana Deus Clement Sangu amesema kuwa kikao hiki ni kinatoa fursa ya kuweka msisitizo wa uzingatiaji wa Sheria,Kanuni,Taratibu na Miongozo katika usimamizi wa Rasiliamali watu katika Utumishi wa Umma.
Na kuongeza kuwa pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Serikali lakini bado kumeendelea kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya Watumishi ambayo kwa kiasi kikubwa yanafanana na mengine ni ya muda mrefu na yapo katika dhamana ya waajiri kisheria.
“Mheshimiwa Mgeni, kikao hiki kinatoa fursa ya kuweka msisitizo wa uzingatiaji wa Sheria,Kanuni,Taratibu na Miongozo katika usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma na kutolea maelekezo muhimu kwa washiriki kuhusu masuala mbalimbali ya utawala na usimamizi wa Rasiliamali watu katika Utumishi wa Umma, kuweka maazimio mbalimbali ya kiutendaji kwa lengo la kuboresha zaidi utawala na usimamizi wa Rasiliamali watu katika Utumishi wa Umma, kueleimisha juu ya masuala mtambuka yanayohusu Afya ya Akili,fursa za uwekezaji kwa watumishi wa umma na umuhimu wa maadili katika kuweka mazingira bora ya usimamiz wa Rasilimaliwatu katika utumishi wa umma “.
“Kote nilikoweza kufika nimeshuhuudiia kazibkubwa ambayo iimeeendelea kufanywaa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raisi wetu mpendwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan hususani katika kubrrsha maslahi pamoja na mazingira mazuri ya kazi kwa watumishi wa Serikali. Aidha pamoja na kazi nzuri ambayo inafanywa na Serikali yetu lakini bado kumeendelea kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya watumishi ambayo kwa kiasi kikubwa yanafanana na mengi nibya muda mrefu na yapo katika dhamana ya waajiri kisheria”.
Kikao kazi kimeshajihishwa na kauli mbiu inayosema :”Kusimamia Sera na Sheria za Utumushi wa Umma kupitia Mifumo ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala ya Kidijitali iliyoboreshwa”.