Zanzibar: CAG amewataka watumishi wanapofanya kazi ya ukaguzi kuwa waelekezaji badala ya kukemea

Na Nihifadhi Issa.

MAKAMU Mwenyekiti wa Bodi ya Utumishi Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar (CAG), Dk Idrissa Muslim Hija amewataka watumishi wa ofisi hiyo wanapofanya kazi ya ukaguzi kuwa waelekezaji badala ya kukemea.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano mkuu wa ofisi hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya ukaguzi kisiwani hapo, amesema wakati mwingi yapo yanayofanyika kwa nia njema ila kwasababu ya uelewa au kukiuka taratibu inaweza kuonekana mtu kafanya vibaya lakini kumbe ni namna ya kumuelekeza kuzingatia utaratibu.

“Tunapowakagua watendaji tuwe waelekezaji zaidi badala ya kuwakemea, tunafanya kazi na watu ambao wengi wetu wanafanya kazi kwa malengo mazuri ya kuendeleza nchi yetu,” amesema

Ametumia fursa hiyo kuwataka wawe na lugha nzuri kwa wanaowakagua “lugha nzuri ni kitu muhimu sana, ila kwa kukosa lugha nzuri unashindwa kupata unachokitaka kwasababu ya kutumia lugha yenye ukakasi.”

Mbali na kuwataka kuwa waelekezaji na kutumia lugha ya stara, kadhalika amewataka watendaji hao kuwa wabunifu, waadilifu na kujifunza mbinu mpya katika utendaji kazi ili kuleta ufanisi wa kuimarisha rasimali za umma.

“Weledi katika kazi hii ya ukaguzi ni muhimu sana hasa katika kuwasilisha yale ambayo umeyafanyia kazi kwa wale mnaowakagua na ngazi mnayopeleka ripoti hiyo,” amesema

Amesema kazi za udhibiti zitasababisha katika mafaniko na uwajibikaji na hatimaye kuleta tija kwa wananchi.

Zimefanikiwa kuchochea utoaji wa huduma za jamii, elimu afya maji safi na salama na umeme na hudUma zinginezo.

Naibu CAG, Khamis Juma amesema kazi za ukaguzi wa rasimali za umma zimefanikiwa kuchochea kuimarika huduma za kijamii ikiwemo elimu afya, maji safi na salama.

Amesema awali walikuwa na programu ya siku ya ukaguzi sasa wameona waende mbali wawe na wiki ya ukaguzi kutambulisha ofisi zaidi kitaifa na kimataifa.

Amesema katika wiki ya ukaguzi wanafanya shughuli mbalibali, kuwatembelea watoto wenye mahitaji wazee na kufanya usafi na kutoa elimu kwa jamii ikiwa ni sehemu ya kutambulisha zaidi ofisi hiyo na majukumu yake.

“Kinachoendelea ni kutoa taaluma mbalimbali, kwasasa tumesema katika wiki ya ukaguzi tumesema kuwe na mkutano mkuu ambao utakuwa na uwasilishaji wa mada kunyesha tulipotoka na tunapoelekea kuangalia changamoto na namna tunavyokwenda mbele,”

Ofisa Mdhamini, Hamad Khamis Mselem amesema hiyo itawasaidia kurekebisha yale ambayo walipanga mwaka uliopita lakini hawakuyafikia ili wayakamilishe na tena kwa ufanisi mkubwa.

Maadhimisho ya wiki ya ukaguzi yanaumuhimu katika usimamizi wa rasilimali za umma, kuimarisha utawala bora, kuleta nidhamu, uwajibikaji na kuongeza uwazi katika usimamizi wa rasimali za umma.

Related Posts