Na Khadija Kalili, Michuzi Tv
BODI ya korosho CBT kwaniaba ya serikali zimesambaza viuatilifu vya zao la korosho aina ya salfa ya unga Tani 19000 na salfa ya maji lita 64000 kwa wakulima wa Mkoa wa Pwani.
Katika msimu wa kilimo wa mwaka 2023/2024 na kuleta ongezeko la asilimia zaidi ya 30 ya uzalishaji wa korosho Mkoani Pwani.
Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Bodi ya korosho CBT tawi la Dar es salaam Domina Mkangara wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Maonyesho ya 4 ya uwekezaji na Viwanda Mkoa wa Pwani Kibaha Mkoani Pwani.
Amesema usambazaji wa viwatilifu hivyo kwa Wakulima ndio umeleta tija katika uzalishaji wa korosho katika mavuno ya mwaka huu 2024 na kufikia Tani 21000 huku makusanyo yakiwa yanarndelea katika Mkoa wa Pwani.
Domina alisema pia mbalimbali ya makusanyo hayo yakupitia Vyama vya msingi vya Wakulima Amcos lakini pia Wakulima Wakulima na wafanyabiashara wadogowadogo wanabangua korosho kwa ajili ya kuendelea kunufaika na ongezeko hilo uzalishaji wa korosho Mkoani Pwani.
Amesema Mkoa wa Pwani nimiongoni mwa mikoa kikubwa inayozalisha korosho hapa nchini lakini mwaka huu kumekuwa na mabadiliko makubwa ya uwekezaji husussni kupitia uwekezaji wa viwanda ambapo mkoani humo Kuna uwekezaji mkubwa wa kiwanda kikubwa Cha ubanguaji wa korosho ambacho kinazalisha Tani 10000 za korosho kwa mwaka huko Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
“Lakini pia kiwanda hicho kikubwa kinazalisha mafuta ya ganda la korosho kwa wingi kwa kutumia teknolojia za kisasa ukilinganishs na maeneo mengine ambayo yana viwanda vidogo kwaajili ya ukamuaji wa mafuta ya ganda la korosho”
“Kama wote tunavyotambua kwamba katika zao la korosho asilimia mia Moja ya kila kinachozalishwa kinatumika na ndio uwekezaji huu ambao tunaweza kuuona kwa bidhaa mbalimbali”
“Bodi ya Korosho inahamasisha katika uwekezaji upande wa viwanda ambapo kwasasa kuna kongani la Viwanda kule Nanyamba Mkoani Mtwara ambapo uendelezaji wake upo katika hatua mbalimbali kwani serikali imeendelea kuwezesha ili huo mradi uweze kukamilika ili hadi kufikia mwaka 2030 korosho inayozalishwa nchini ikibanguliwe hapa hapa nchini” anesema Domina.