Rais Samia na Dr. Leakey kutunukiwa Tuzo Arusha

Tanzania inatarajia kuzindua Tuzo za Kitaifa za Utalii na Uhifadhi Desemba 20, 2024, ikiwa ni hatua ya kutambua na kuenzi mchango wa wadau wa sekta hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan atatunukiwa tuzo ya heshima kwa mchango wake kupitia filamu za Royal Tour na Amazing Tanzania. Dk. Louis Leakey na Mary Leakey pia watatuzwa kwa uvumbuzi wa fuvu la Zinjanthropus na nyayo za Laitori ambazo zimeendelea kuvutia maelfu ya watalii.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbasi, amesema tuzo hizo zitatolewa kila mwaka kwa lengo la kuimarisha utalii na uhifadhi nchini.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongozana na viongozi mbalimbali wa serikali na wadau wa utalli.

Burudani kutoka kwa wasanii kama Weusi, Frida Amani, na vikundi vya India na China zitaongeza mvuto wa tukio hilo.

Tuzo hizi ni ishara ya kuthamini sekta zinazochangia pato la Taifa kupitia fedha za kigeni.

Related Posts