VIDEO: Askari polisi wawili wauawa wakikamata mtuhumiwa

Dodoma. Askari polisi wawili wameuawa usiku wa kuamkia leo Desemba 18, 2024 kwa kushambuliwa na mtuhumiwa wa unyang’anyi wa kutumia silaha, Atanasio Malenda, wakati walipokwenda kumkamata nyumbani kwake.

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Msagali wilayani Mpwapwa Mkoa wa Dodoma, katika tukio ambalo Malendo (30) naye ameuawa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, George Katabazi, tukio hilo limetokea saa 7 usiku wa kuamkia leo Jumatano, Desemba 18, 2024 wakati askari D/koplo Jairo Boniface Kalanda na Pc Alfred John walipokwenda kumkamata mtuhumiwa huyo.


Askari polisi wawili wauawa wakikamata mtuhumiwa

Amesema askari hao waliuawa kwenye mapambano ya risasi na mtuhumiwa, akidaiwa alikuwa ametoka kumjeruhi Yohana Lameck na kumpora Sh2 milioni.

Kwa mujibu wa Kamanda Katabazi, Malenda alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa mapambano hayo.

Katika majibizano hayo, pia D/Koplo Msuka na mwananchi mmoja, Masima Nyau walijeruhiwa na wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts