Vifo ajali ya Coaster, lori Morogoro vyafikia 15

Morogoro. Mtu mmoja amefariki dunia, na kufanya idadi ya vifo kufikia 15, kufuatia ajali ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Coaster kugongana na lori katika eneo la Mikese, barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Mganga mkuu Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, Daniel Ngungu leo Jumatano Novemba 18, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Dk Daniel amesema usiku wa jana walipokea miili 14 hospitalini hapo ambapo minane ilikuwa ya wanaume na sita ni ya wanawake.

Habari kutoka eneo la tukio, zinadai chanzo cha ajali ni dereva wa lori lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kutaka kuyapita magari yaliyo kuwa mbele yake pasipo kuchukua tahadhari.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts