Jukwaa
linaloongoza kwa huduma ya usafiri nchini Tanzania Bolt, limetoa tahadhari kali
kwa abiria na madereva kujiepusha na safari za nje ya mtandao. Tahadhari hii
inakuja kama sehemu ya dhamira inayoendelea ya Bolt ya kuhakikisha usalama wa
abiria na madereva kwenye jukwaa lake.
Usafiri
unaopangwa nje ya mtandao wa Bolt uhatarisha usalama mkubwa kwa madereva na
abiria, pia utakuwa unakwepa hatua za usalama za ndani ya mtandao wa Bolt,
ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa safari, uthibitishaji wa utambulisho na
mifumo ya usaidizi wa dharura.
Dimmy
Kanyankole, Meneja Mkuu Bolt Tanzania alisisitiza
umuhimu wa kuzingatia mifumo ya mtandao wa Bolt kwa abiria wote “Kwa Bolt,
usalama ni kipaumbele chetu cha juu. Safari za nje ya mtandao hudhoofisha vitengo
vya usalama tulivyonavyo ili kulinda watumiaji wetu, kama vile ukaguzi wa
magari, ufikiaji wa taarifa za dharura na kujua mahali ulipo kwa wapendwa wako ukiwa
safarini. Tunawashauri sana madereva na abiria wetu kutumia programu ya Bolt
kwa safari zao zote ili kuhakikisha usalama wao. Kwa kuweka safari ndani ya
mifumo yetu ya mtandao, watumiaji wanahakikishiwa usalama ambao mfumo wetu
hutoa.”
Vitengo vya
usalama vya ndani ya programu ya Bolt ni pamoja na:
● Shirikisha Eneo
Ulipo: Abiria na madereva wanaweza kushirikisha mahali walipo kwa wakati
halisi na maelezo ya safari—kama vile kuchagua gari, muundo, nambari ya usajili
na kujua eneo ulipo kwa salama kwa kutumia kiongoza safari.
● Usaidizi wa
Dharura: Katika hali ya dharura, abiria na madereva wanaweza kutahadharisha
timu ya kushughulikia dharura kwa haraka na kwa uangalifu kwa kutumia kitufe
cha Usaidizi wa Dharura wa ndani ya programu. Kipengele hiki pia huarifu timu
ya usalama ya Bolt, ambayo itapiga simu ya haraka ili kuhakikisha hali hiyo
inashughulikiwa mara moja.
● Kukagua
Safari: Timu ya usalama ya Bolt hufuatilia safari kwa makini ili kugundua
jambo lolote lisilo la kawaida wakati wa safari, na kuhakikisha kwamba itashughulikia
suala lolote kwa wakati linapohitajika.
● Msaada wa
Usalama kwa muda wote: Timu yetu ya usalama iliyojitolea inapatikana kila
saa ili kutoa msaada wakati wa safari na
baada ya safari.
Abiria
wanahimizwa kuripoti tabia yoyote ya kutiliwa shaka au isiyofaa kupitia program
zetu kwa uchunguzi wa haraka. Bolt inasalia na nia ya kutengeneza hali salama
na ya kuaminika isiyo na mashaka ya usafiri kwa watumiaji wote nchini Tanzania.
Kampuni itaendelea kuwekeza katika vitengo vya usalama na kampeni za
uhamasishaji kwa umma kushughulikia masuala ya usalama katika sekta ya usafirishaji.