Timu ya Kigoma imeifunga Foundation Pax kwa pointi 89-82, katika mchezo wa kirafiki wa ujirani mwema, uliofanyika kwenye Uwanja wa Lake Side, mkoani humo.
Akiongea na Mwanaspoti kwa simu kutoka Kigoma, Katibu mkuu wa chama cha mpira wa kikapu mkoani humo, Kibonajoro Anasi alisema mchezo huo ulikuwa ni wa pili kufanyika tangu mara ya kwanza mwaka 2022 na Foundation Pax iliibuka washindi.
“Hii ni heshima kwa nchi yetu, kwa timu ya Mkoa wa Kigoma kuishinda Faundation Pax mwaka huu,” alisema Anasi.
Anasi ambaye pia ni kocha wa timu ya mkoa huo, alisema ushindi wao umetokana na mafanikio ya mkoa kwa mwaka 2024.
“Mafanikio yametokana na jinsi mkoa huu, ulivyoibua vipaji kwa vijana wa umri mdogo, pamoja na kubeba Taifa Cup mwaka huu,” alisema Anasi.