Lukuba: Outsiders tulizingua wenyewe | Mwanaspoti

MWEKAHAZINA wa  UDSM Outsiders, Rama Lukuba ameshindwa kujizuia na kusema kilichoiua timu hiyo na kushindwa kubeba ubingwa wa ligi ya kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL) mwaka huu, ni wao tu.

Akiongea  na Mwanasposti katika viwanja vya Donbosco Upanga,  Lukuba alisema nafasi waliyopata mwaka huu haiwezi ikajirudia tena.

Alisema timu hiyo ilikuwa na kikosi kizuri na ilionyesha kiwango kikubwa mizunguko miwili ya mwanzo, robo fainali na nusu fainali na  waliamini itatwaa ubingwa kabla ya mambo kugeuka.

Alisema kikosi hicho kilikuwa na wachezaji wazuri na kama ingewatumia vizuri katika mchezo wa fainali ubingwa ungeenda kwao.

“Tulikuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa, lakini hatukuwatumia katika fainali,” alisema.

Aliwataja wachezaji hao ni Jimmy Mollel, Sabibi, Evance Davies na Mwalimu Heri.

Fainali hiyo ilichezwa kwa timu kucheza michezo mitano ‘best of five play off’ na JKT ilishinda michezo 3-1.

UDSM iliyotinga katika fainali hiyo kwa mara ya kwanza tangu ilipoanzishwa, katika mzunguko wa pili ilishika nafasi ya pili kwa pointi 54.

Nafasi ya kwanza ilienda kwa Dar City iliyopata pointi 55, huku JKT ikiwa ya tatu kwa pointi 51.

Related Posts