Meneja Mtendaji wa Mr.Uk Deo Joachim Kusare akionesha bidhaa ya jiko la kisasa la gesi kwenye maonesho hayo anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa Hoteli ya Rolex Constancia Makoye
Na Mwandishi Wetu
MKOA wa Pwani unatarajia kuwa na kiwanda cha kutengeneza majokofu hii ikiwa ni katika kukuza uchumi wa viwanda.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda ya Mr.UK Tanzania ambaye ni kati ya washiriki wa Wiki ya Maonesho ya Viwanda biashara na uwekezaji yanayoendelea kwenye viwanja vya Stendi ya zamani Mailimoja Wilayani Kibaha Mkoani Pwani
Meneja Mtendaji wa Kampuni Deo Joakim Kusare amesema kuwa wanatarajia kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza majokofu ambacho kitakua Kerege Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani ndani ya miaka miwili ijayo na tayari ujenzi wa wa kiwanda hicho umeanza
Hivi sasa Mr.UK ni Kampuni kubwa na maarufu kutokana na biashara yake ya kuuza bidhaa mbalimbali za vifaa vya ndani vinavyotumia umeme.
“Biashara zetu zimejikita kwenye kukidhi haja kwa watu wa kada zote za kipato na hadi sasa runefanikiwa kutoa ajira nyingi kwa vija a nchini”amesema Meneja Kusare.
Amesema kuwa hivi sasa wanachukua malighafi kutokanje ya nchi na wanamiliki katakana ndogo iliyopo maeneo ya Tandale Jijini Dar es Salaam.
“Hivi sasa tunachukua malighafi nje ya nchi kisha tunakuja kuunganisha kwenye katakana yetu iliyopo Tandale amezitaja baadhi ya bidhaa wanazounganisha kuwa ni sabufa,sound bar AC,Majokofu pampu za kilimo pamoja na majiko ya gesi yanayotumia kiwango kidogo cha gesi.
Kusare amesisitiza kwa kusema kuwa vifaa vyao vinapatikana kwa bei nafuu pia vinatumia umeme mdogo.
Wakati huohuo Meneja Masoko wa Hotel Rolex Constancia Makoye amesema mbali ya bidhaa hizo kesho tarehe 20 Desemba, 2024 watazindua hoteli yenye hadhi ya nyota tano itakayo fahamika kwa jina la Rolex ambayo iko Dar es Salaam.