SERENA YAKARIBISHA SIKUKUU YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA NA WATOTO YATIMA DAR

TAASISI, Kampuni na Mashirika yakumbushwa kurudisha Kwa jamii kile wanachokipata kutoka kwa wateja ili waweze kuifikia jamii kwa watu wenye uhitaji kwenye Jamii inayowazunguka.

Akizungumza hayo Meneja Rasilimali watu Frolentina Ninnah kutoka Hoteli ya Dar es Salaam Serena wakati wa Kukaribisha Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya kwa watoto yatima waliojumuika hotelini hapo amesema bado kunahitaji nguvu kubwa kwa Taasisi, Makampuni na Mashirika kuona nafasi ya Kusherehekea sikukuu hizo na watoto yatima ambao wanahitaji faraja zaidi.

“Sisi Kama Kampuni tumeona kila mwaka turejeshe kwa jamii hasa kwa watoto ambao wanahitaji faraja ukizingatia tunaelekea Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya ambapo tunaamua kuigusa jamii kuhakikisha tunajumuika nao katika kula chakula cha pamoja na kuwapa Mahitaji mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule na chakula kwa ujumla lakini bado haitoshi kwa sisi peke yake tunaomba na wenzetu waguswe kwa hili tunachokifanya ili waweze kufanya zaidi ya hiki kwani vituo vipo vingi zaidi”.

Hata hivyo amesema Kwa Mwaka huu wameweza Kusherehekea na Watoto zaidi ya 100 kutoka vituo viwili vyenye Uhitaji Jijini Dar es Salaam.

Aidha Kwa Upande wake Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima Malaika Kids , Khadija Said ametoa pongezi kwa uongozi wa hoteli hiyo kwa kuwapa faraja Watoto hao wenye Uhitaji katika vituo vya kulelea .

Hata hivyo ameomba watu wengine wenye uwezo wakiwemo Makampuni ,taasisi na Mashirika kutembelea vituo hivyo kuhakikisha wanawapatia mahitaji mbalimbali .

Related Posts