TRC yaongeza treni ya abiria Kilimanjaro, Arusha

Moshi. Kufuatia wingi wa abiria wanaokwenda mikoa ya Kaskazini hususan Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeongeza safari moja ya treni ya abiria kuelekea mikoa hiyo.

Treni hiyo itaanza safari zake kutoka Mkoa wa Dar es salaam kwenda Kilimanjaro Jumamosi Desemba 21, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa kitengo cha uhusiano wa shirika hilo, Fredy Mwanjala treni hiyo itaondoka Jijini Dar es salaam Desemba 21 saa 8:30 mchana kuelekea Kilimanjaro na Arusha na itaondoka Arusha Desemba 22  saa 8:30 mchana kuelekea Kilimanjaro na Dar es salaam.

“Shirika la reli Tanzania (TRC) lina utaarifu umma kuwa kutokana na ongezeko la abiria wanaohitaji kusafiri na treni kuelekea Kilimanjaro na Arusha, shirika limeongeza treni moja ya abiria kuelekea mikoa hiyo Jumamosi Desemba 21,” imeeleza taarifa hiyo.

Related Posts