WAZIRI MASAUNI: SERIKALI IMEPIGA HATUA USIMAMIZI WA MAZINGIRA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi, Hamad Yusuf Masauni alipokwenda kujitambulisha kwake

……

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema Serikali imepiga hatua katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira licha ya changamoto zinazojitokeza. 

Ameyasema hayo Desemba 18, 2024 alipokuwa kwenye ziara ya kikazi Zanzibar na kuongeza kuwa ushirikiano wa viongozi wa Ofisi ya Makamu wa Rais umeleta tija katika sekta ya mazingira.

“Nina siku chache tangu nimeingia katika wizara hii lakini najiona mtu mwenye bahati kwani kwa muda mfupi tangu nimekuja nimejifunza vitu vingi kama nimekaa miaka miwili na hii inatokana na kuwepo kwa timu nzuri kwani ni watu wenye kasi katika utendaji wao wa kazi,” amesema. 

Mhandisi Masauni amesema ingawa suala la mazingira si la Muungano linapokuja suala la uwakilishi, wananchi wa Zanzibar wanalitegemea kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuweza kupata fursa mbalimbali hivyo mipango thabiti inahitajika kwa maslahi ya nchi. 

Aidha, kuhusu Uchumi wa Buluu Mhe. Masauni amesema ushirikiano utaendelea baini ya pande zote mbili kati ya Tanzania Bara na Zanzibar ili kufungua zaidi milango ya uwekezaji katika eneo hilo. 

“Mafanikio ambayo yanaonekana kwenye eneo la Uchumi wa Buluu ni ishara tosha kwamba tumeanza kupiga hatua hivyo tutaendelea kuliboresha na zile changamoto ambazo zimejitokeza kwa pamoja tunaendelea kuzipatia ufumbuzi,” amesema Mhe. Masauni. 

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akifanya jitihada mbalimbali katika eneo hilo ikiwemo upatikanaji wa fedha kwa njia mbalimbali hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kutoa ushirikiano ili kufanya eneo hilo kupiga hatua zaidi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana kwenye mambo mbalimbali hususan ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira. 

Amesema hauwezi kuzungumzia Uchumi wa Buluu bila kugusa mazingira huku akisitiza kuwa muhimu ni kubadilishana uzoefu ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa viongozi na wananchi kuhusu suala hilo.

Nae Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi wa Zanzibar Mhe. Shabaan Ali Othman amesema eneo hilo linahitaji ushirikiano mkubwa ili kufanikisha malengo ambayo kila mtu anatarajia kuyaona yakipatikana katika eneo hilo hasa katika kutatua changamoto zilizoto na zitakazojitokeza.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia) akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi, Hamad Yusuf Masauni alipokwenda kujitambulisha kwake

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi, Hamad Yusuf Masauni (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Harus Said Suleiman alipokuwa katika ziara ya kikazi Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi, Hamad Yusuf Masauni (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi Mh.Hamza Hassan Juma  alipokuwa katika ziara ya kikazi Zanzibar, Desemba 18, 2024.

Viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi, Hamad Yusuf Masauni (aliyekaa mbele kushoto) alipokuwa akizungumza masuala mbalimbali kuhusu Uchumi wa Buluu katika ziara yake Zanzibar, Desemba 18, 2024.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akizungumza katika kikao cha kujadili masuala mbalimbali kuhusu Uchumi wa Buluu kilichofanyika Zanziba, Desemba 18, 2024.

Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mtawi (aliyesimama) akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi, Hamad Yusuf Masauni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hamza Hassan Juma, Desemba 18, 2024.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi, Hamad Yusuf Masauni (wa pili kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Harus Said Suleiman (wa nne kulia) wakiwa katika picha na viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais  na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi, Hamad Yusuf Masauni (wa pili kushoto) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Harus Said Suleiman (wa nne kulia) wakiwa katika picha na viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais  na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

Related Posts