Mwili wa Ulomi wawasili kijijini kwao, maziko leo

Siha. Mwili wa mfanyabiashara Daisle Ulomi umewasili nyumbani kwao, kitongoji cha Kikwe, Kata ya Nasai, Sanya Juu, wilayani Siha kwa ajili ya maziko yanayofanyika leo Desemba 20, 2024 katika makaburi ya familia.

Ulomi, mfanyabiashara wa huduma za kifedha kupitia mitandao, alipata ajali Desemba 11 jijini Dar es Salaam na mwili wake ulitambuliwa na famiia Desemba 16, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.

Baada ya mwili kufikishwa nyumbani, utapelekwa kanisa kwa ibada na baadaye utarejeshwa kwa ajili ya maziko.

Desemba 17, 2024 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alitoa taarifa kuhusu kifo cha Ulomi ambaye awali ilielezwa alitoweka alipokuwa ofisini kwake Sinza Kijiweni.

Eneo la kaburi utakapozikwa mwili wa Daisle Ulomi kwenye makaburi ya familia katika kitongoji cha Kikwe, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

Kamanda Muliro alifafanua kuwa Ulomi alipata ajali akiwa kwenye pikipiki yake kwa kugonga lori kwa nyuma katika Barabara ya Mandela na kusababisha kifo chake.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts