Rais Mwinyi: Zanzibar ipo tayari kwa mashindano ya Chan 2025

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amelihakikishia Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘Caf’ kuwa Zanzibar ipo tayari na inajiandaa vema kufanikisha Mashindano ya ‘Chan’ yanayotarajiwa kufanyika Februari mwakani.

Rais Dk.Mwinyi aliyasema hayo alipozungumza na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe aliefika Ikulu Zanzibar jana 19 Desemba.

Aidha , Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inaendelea na Ujenzi wa Miundombinu ya Viwanja kwa kasi kubwa ili ikamilike kwa wakati na kufanikisha Mashindani hayo na kuishukuru CAF kwa Kuiamini Zanzibar.

Rais Dk.Mwinyi alisisitiza kuwa mbali na viwanja pia Serikali inajiandaa na kuwa na hoteli bora na za kutosha zitakazokuwa na uwezo wa kupokea wageni watakaofika kwa ajili ya mashindano hayo na huduma bora.

Naye, Rais wa CAF Patrice Motsepe alieleza kufarijika na maandalizi ya Kiwanja cha New Amani Complex na utayari wa Zanzibar kufanikisha mashindano hayo.

Halikadhalika Rais Motsepe alisifu juhudi zinazoendelea za kuimarisha viwanja vya ndege , miundombinu ya barabara na ongezeko la hoteli mambo aliyosema kuwa ni muhimu katika kufanikisha Mashindano.

Related Posts