Serikali yazindua nyumba 109 za waathirika Hanang

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 20, 2024 amezindua na kukabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 03, 2023 Hanang, Mkoani Manyara.

Nyumba hizo ambazo zimejengwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) zipo katika kijiji cha Wareti, Wilaya ya Hanang mkoani Manyara.

Ujenzi wa nyumba hizo ulitokana na maamuzi ya Rais Dkt. Samia baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa na maporomoko ya tope. Uamuzi huo ni muendelezo wa dhamira ya dhati ya Serikali ya kuwalinda wananchi wake na kurejesha hali ili waendelee na mfumo wa maisha baada ya maafa.

 

Related Posts