Shinyanga. Gari aina ya Toyota Harrier lililobeba watu sita wa familia moja limepinduka baada ya kuacha njia na kuingia kwenye mtaro.
Ajali hiyo imetokea leo Desemba 20, 2024 eneo la Kizumbi katika Manispaa ya Shinyanga, saa 9 mchana.
Mmoja ya waathirika wa ajali hiyo, Diana Willibard amesema gari hilo ilianza kupata shida wakiwa Tinde.
“Tulikua tunatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza tulivyofika Tinde gari likapata shida na kuzima, hivyo tukaomba msaada wa gari lingine aina ya Toyota Noah kutuvuta ili kutusogeza eneo ambalo tutapata msaada.
“Tulipofika eneo la Kizumbi bomba lililofungwa kutuvuta likakatika na gari likapinduka na kuingia kwenye mtaro,” amesema Diana.
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kwamba, askari wamekwenda eneo la tukio.