TGNP yasherehekea miaka 30 ya Beijing, yahimiza wanawake kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi ujao

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umesherehekea miaka 30 ya Beijing katika kongamano la wanawake na uongozi Dar es Salaam leo huku ukihimiza umuhimu wa wanawake kuendelea kujitokeza kwa wingi  katika uchaguzi mkuu ujao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi amesema wanayo furaha kuona uchaguzi wa serikali za mitaa namna wanawake wengi wameitikia na kushika nafasi za wenyeviti akisema anaamini data zitaendelea kuongezeka.

 kwenye uchaguzi wa 2019 ni madiwani, na kwamba asilimia 2.1 ya wanawake wali

“Tunayo imani kwamba kuna uchaguzi wa mwaka ujao data zitakuwa tofauti lakini hapa tunayo mifano ya wanawake waliopasua miamba kwenye uchaguzi uliopita,”amesema.

Rais wa kwanza wa Bunge la Afrika Getrude Mongella ambaye pia, aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Beijing  amesema kuelekea katika uchaguzi mkuu ujao wagombee wanawake watafutwe walio sahihi.

“Tutafute watu sahihi, tuwape moyo ili mwakani hiyo asilimia kubwa tunayoitafuta tuwe nao. Na pia tuendelee kutoa michango ya Mawazo na vitendo na kujitolea katika kuhakikisha tunakamilisha hayo mapinduzi,”amesema. 

Amesema kazi hiyo sio nyepesi inahitaji kujengwa katika dira ya miaka 50 ili hatua zifuatwe taratibu na kuwe na kupokezana vijiti baada ya muda fulani.

Mwenyekiti wa Bodi wa TGNP Gemma Akilimali amesema ana furaha kubwa kwa kuwa kongamano lao limefanyika baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa  ambap mwaka huu wanawake wamepata hamasa kubwa ya kushiriki katika kinyang’anyiro cha uchaguzi.

Amesema pamoja na changamoto mbalimbali lakini wapo wengi waliopata uongozi, kuna maeneo ambayo wanawake wameshika nafasi ya wenyeviti wa serikali za mitaa kwa mara ya kwanza

“Hili ni jambo la kujivunia na kusherehea. Tukumbuke kuwa 2025 tunaadhimisha miaka 30 tangu kufanyike mkutano mkubwa wa wanawake duniani uliofanyika Beijing hivyo, kama sehemu ya kusherehekea leo tupo na wanawake walioshiriki miongoni mwao ni  Zakia Meghji, Ruth Meena, Eda Sanga, Hellen Bisimba na wengine,”amesemawanawake mbalimbali walio katika nafasi mbalimbali za uongozi hususani viongozi wa kisiasa ili waweze kushirikishana uzoefu.









Related Posts