TRA yawashukuru walipa kodi wa Mbinga

 

 

Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo amesema kuwa ulipaji wa kodi ndio maendeleo ya Taifa lolote duniani.

Kayombo aliysema hayo katika mkutano na Wafanyabiashara wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma uliofanyika  katika ukumbi wa FDC.

Kayombo amewashukuru wafanyabiashara hao kwa kuendelea  kulipa kodi zao kwa hiari na kwa wakati na kuuwezesha Mkoa wa Ruvuma na Taasisi kwa ujumla kuvuka malengo yaliyopangwa na serikali. 

Ameaema sambamba na  kuwashukuru Wafanyabiashara pia amewataka kuendelea  na tabia hiyo ya ulipaji wa kodi.

Kayombo amekata keki na kuwalisha viongozi wa wafanyabiashara na wafanyabiashara wengine.

Pia amewahamasisha Wafanyabiashara wa Mkoa wa Ruvuma walipe kodi zao za awamu ya nne mapema kabla ya tarehe 31/12/2024.

 

Related Posts