BARABARA YA ITONI-LUSITU HAIJATELEKEZWA,RASILIMALI ZILIENDA KUSAIDIA MAENEO HATARI – MBUNGE MWANYIKA


Wakati wasiwasi ukitanda kwa wananchi wa halmashauri ya mji wa Njombe na Ludewa kutokana na mkandarasi anayejenga barabara kuu ya kuelekea wilayani Ludewa kipande cha Itoni – Lusitu kwa kiwango cha zege kusimama ujenzi kwa takribani mwaka mmoja mpaka sasa,Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Deodatus Mwanyika amewatoa hofu wananchi na kueleza kuwa ujenzi utaendelea baada ya mvua kuisha.

Mwanyika akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2020-2024 kwa jimbo la Njombe mjini amesema wapo watu wanaosema barabara hiyo imetelekezwa jambo ambalo sio la kweli lakini ujenzi ulisimama kwa kuwa baadhi vifaa na rasilimali fedha ilihamishwa na kwenda kusaidia kutatua changamoto kwenye maeneo mengine yaliyokuwa hatari kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mwaka jana.

“Barabara hii ilikuwa ijengwa kwa miaka miwili na ujenzi wake ulianza haraka sana lakini kwa bahati mbaya kwa kipindi cha mwaka mmoja mkandarasi hayupo site na nitoe sababu kwa kuwa kuna watu wanawaza barabara hii imetelekezwa niwaambie barabara hii haijatelekezwa,sote ni mashahidi mwaka jana kulikuwa na mvua zisizo za kawaida lakini Njombe mjini hatukuona sana hizo mvua na madhara yake lakini wenzetu Kibiti,Lindi,Mafya maji yalikuwa kwenye mapaa ya nyumba”amesema Mbowe.

Mwanyika amesema mara baada ya hali hiyo serikali ilifanya maamuzi ya kusaidia wananchi kwenye maeneo yaliyokuwa yamepata tatizo kubwa kwa kupunguza kasi ikiwemo kuondoa baadhi ya vifaa na rasilimali fedha kwenda kutatua changamoto kwenye maeneo yenye shida kubwa.

“Kwa hiyo ndugu zangu barabara hiyo ilisimama kwasababu hizo sio kwa kutelekezwa ila ni kwasababu ilionekana rasilimali ziende kusaidia maeneo ambayo yamekuwa ni hatari na tunashukuru Waziri wa Ujenzi ametuhakikishia kuwa kipindi hiki fedha zitaletwa kwa hiyo tunauhakika mvua zikiisha mkandarasi ataendelea na kazi”amesema Mwanyika.

 

Related Posts