Iringa yavuka lengo la ukusanyaji mapato kwa asilimia 106 ndani ya miezi 5

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Iringa imewashukuru walipa kodi kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa kipindi cha miezi 5 ambapo imekusanya kwa asilimia 106.

Akizungumza katika hafla ya kutoa shukrani kwa mlipa kodi kwa kutimiza wajibu Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Iringa Peter Eliona amesema kuwa lengo lilikua ni kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 21 badala yake imekusanya shilingi Bilioni 22 ikiwa ni sawa na asilimia 106%.

Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nchini, Ephraim Mdee ambae pia ni Mkurugenzi wa utafiti sera na mipango amefafanua kwamba Wafanyabiashara Mkoani Iringa wamefanikiwa kulipa kodi kwa asilimia 106 kwa kipindi cha miezi mitano kuanzia Julai hadi November 2024 huku akieleza kuwa hatua hiyo ni ishara ya na ufanisi wa wafanyabiashara wa mkoa huo katika kutimiza majukumu yao ya kisheria ambapo mafanikio hayo yana mchango mkubwa katika kufanikisha malengo ya serikali ya kukuza uchumi wa taifa na kuboresha huduma za kijamii.

“Mchango wa Wafanyabiashara ni Muhimu kwa Uchumi na haya yanaonyesha jinsi Wafanyabiashara wa Iringa mnavyotambua umuhimu wa kulipa kodi na mchango wenu katika maendeleo ya taifa “

         

Related Posts