Simba kwa penalti, acha kabisa!

SIMBA ipo uwanjani jioni ya leo mjini Bukoba kuvaana na Kagera Sugar katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara, huku rekodi zikionyesha timu hiyo pamoja na nyingine tatu za Namungo, Coastal Union na Tabora United ndizo vinara wa kupata penalti na kuzitumia kuwapa matokeo chanya.

Lakini timu hizo nne zikifunika kwa kupata penalti nyingi, wanaoburuza mkia katika ligi hiyo, KenGold imefunika miongoni mwa timu iliyosababisha penalti nyingi hadi sasa ikifanya hivyo mara sita katika mechi 15 ilizocheza.

Hadi sasa zikiwa zimepigwa penalti 36, kati ya hizo ni nne pekee hazikufungwa, huku Simba, Coastal Union, Tabora United na Namungo zikiongoza kwa kupata penalti nyingi kila mmoja ikivuna nne.

Ken Gold kwenye penalti sita walizofungwa ni dhidi ya Mashujaa mfungaji Ismail Mgunda, Azam FC Feisal Salum ‘Fei Toto’, Tanzania Prisons, Jumanne Elifadhili, Namungo Erasto Nyoni akiifunga mabao mawili na Simba Leonel Ateba.

Wakati kwa upande wa Simba ambao wamefunga penalti nne walizipata dhidi ya Coastal Union, Ateba ndio alifunga, vs KMC alifunga Jean Charles Ahoua, wakati dhidi ya Pamba Jiji na Ken Gold mfungaji ni Ateba.

Namungo wao wamefunga dhidi ya Tabora United mara mbili wafungaji Djuma Shaban na Heritier Makambo, Fountain Gate alifunga Moubarack Amza, Coastal Union mfungaji Djuma na dhidi ya Ken Gold wakifunga mabao mawili yote kwa penalti mfungaji Erasto Nyoni.

Kwa upande wa Coastal Union wao pia wamefunga penalti nne dhidi ya KMC, Kagera Sugar mfungaji Maabad Maulid, Tanzania Prisons alifunga Hernest Malonga na dhidi ya Fountain Gate alitupia Lucas Kikoti.

Kinara wa upachikaji mabao Simba, Leonel Ateba ambaye ametupia kambani mara tano, kati ya mabao hayo, matatu amefunga kwa penalti sawa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye amepachika mabao manne hadi sasa kati ya hayo matatu ni ya penalti.

Ateba mabao yake ya penalti amefunga dhidi ya Coastal Union, KMC na dhidi ya Ken Gold, huku Fei Toto akipachika mabao dhidi ya Ken Gold, Kagera Sugar na Dodoma Jiji.

Wenye penalti mbili ni Erasto Nyoni wa Namungo, Jean Charles Ahoua, Morice Chukwu (Tabora United), huku Heritier Makambo na Djuma Shaban (Tabora Utd), Maabad Maulid (Coastal) na Hassan Dilunga (JKT TZ).

Related Posts