Wazazi watakiwa kuwalinda watoto kipindi cha likizo na sikukuu

Mwenyekiti wa Chipkizi Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Morogoro Jeremia Kisena Mabuba amewataka wazazi na walezi kuwalinda watoto na vitendo vya ukatili hasa kipindi hiki Cha likizo na sikukuu.

Mabuba amesema kuwa ataungana na Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha wanakabiliana na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto hasa wakiume ambao wanaonekana wamesahaulika katika jamii kwenye kulindwa na vitendo hivyo.

Mabuba ameyasema hayo wakati akizungumzia na wanadishi wa habari Mkoani humo ambapo amesema kuwa kumekuwa na tabia za kikatili wanazofanyiwa watoto ikiwemo kubakwa,kulawitiwa na kuuawa na kuibwa jambo ambalo halikubariki ni lazima kila Mtu ahakikishe anakuwa mlinzi wa watoto.

Aidha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuwaboreshea bima ya watoto ambayo itawasaidia katika kupata huduma bora za afya.

Katika hatua nyingine ameshukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa madarasa ,kutoa ajira Kwa walimu pamoja kununua vitendea Kazi jambo ambapo linawapa hamasa kuendelea kujifunza zaidi na kupata matokeo mazuri kwenye mitihani.

Amewataka wazazi kuendelea kukiamini chama cham cha Mapinduzi na Serikali kwa ujumla hasa katika ujenzi wa miundombinu ya afya , elimu,barabara, Maji na umeme.

 

Related Posts