Cyprian Kachwele apata uzoefu | Mwanaspoti

MSHAMBULIAJI wa Vancouver Whitecaps ya Canada, Cyprian Kachwele amesema amemaliza msimu salama akiondoka na mambo mbalimbali ikiwemo kupata uzoefu.

Kachwele ni miongoni mwa washambuliaji ambao wamekuwa wakiitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’ akiwa kwenye orodha ya wachezaji walioipeleka Tanzania AFCON licha ya kukaa benchi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kachwele alisema jambo la kushukuru Mungu unapomaliza salama ligi bila majeraha akitaja uzoefu ni jambo kubwa.

Aliongeza msimu uliopita ulikuwa mzuri kwake ambao umemjenga kuwa mchezaji wa aina gani licha ya kutopata nafasi kubwa ya kucheza.

“Unapokuwa kwenye ligi kubwa unakua kiakili, hivyo kama mchezaji unapata uzoefu hasa sisi tunaochipukia kwenye soka, ligi imeisha na natamani msimu ujao uwe bora kwangu,” alisema Kachwele.

Related Posts