DKT.NDUMBARO  ACHAGULIWA MWENYEKITI WA KAMATI MAALUM YA MAWAZIRI WA SHERIA YA UMOJA WA AFRIKA

Waziri wa Katiba na Sheria Nchini Tanzania Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza  maalum la  Mawaziri wa Sheria la  Umoja wa Afrika kikao  kilichowakutanisha Mawaziri, Mabalozi na Wataalamu katika sekta ya Sheria wa Umoja wa Afrika kikao kilichofanyika kuanzia tarehe 14 na kumalizika leo tarehe 22  Desemba, 2024 katika hotel ya Golden Tulip Zanzibar.

Akizungumza wakati akihitimisha kikao hicho kilichodumu kwa muda wa siku kumi
Waziri wa Katiba na Sheria na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Sheria wa Umoja wa Afrika kutoka Nchini Tanzania Mhe.Dkt. Damas Ndumbaro amewashukuru Wajumbe wa Baraza hilo kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi  la Mawaziri wa Sekta ya Sheria kwa Nchi za Umoja wa  Afrika.

“Tumeikubali heshima mliyotupatia Nchi ya Tanzania kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi.Tutafanya kazi kwa pamoja katika kuhakikisha Umoja wa Afrika unakuwa ni sehemu nzuri katika sekta ya Sheria na mfano bora katika utoaji  Haki kwa miaka inayokuja.” Alisema Ndumbaro.

Waziri Ndumbaro amesema kuwa, Kamati za ufundi  za  Wataalamu katika masuala ya Haki na Sheria ni Kamati muhimu katika Umoja wa Afrika ikiwemo kupitia nyaraka ambazo zinatokea katika Kamati za Wataalamu nyingine ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu kwa wakati na usimamizi wa Haki na kuwa makini katika kufanya maamuzi kwa kufanya kazi kwa pamoja ili kufikia maamuzi yenye tija.

Waziri Ndumbaro amewataka Viongozi waliochaguliwa wakiwemo  Makamu Wenyeviti watatu waliochaguliwa na Katibu wa Kamati hiyo  kuhakikisha kuwa wanaanza utekelezaji wa maazimio waliyokubaliana kwa kuunda timu itakayowawezesha kufikisha ajenda kwa vyombo vya maamuzi ili kuweza kutekeleza matakwa ya Umoja wa Afrika.

Related Posts