Mabingwa Misri kumpa dili nono Mtanzania

BAADA ya kufanya vizuri kwenye msimu wake wa kwanza tu wa ligi, Mabingwa wa Ligi ya Wanawake FC Masar imemuandalia dili nono Mtanzania Hasnath Ubamba.

Ubamba alisajiliwa msimu huu kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Fountain Gate Princess ya Tanzania.

Taarifa ilizopata Mwanaspoti kutokea Misri ni timu hiyo iko kwenye mchakato wa kumnunua moja kwa moja Ubamba kutokana na kiwango bora alichoonyesha ndani ya muda mchache tu.

Inaelezwa Masar imeandaa dili nono kwa nyota huyo ambaye amekuwa bora akiwa mhimili mkubwa wa timu hiyo kwenye eneo la kiungo mshambuliaji.

Kama dili hilo litafanikiwa basi Fountain itavuna pesa za kumuuza kwani bado ni mchezaji halali wa timu hiyo iliyopo nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ya Wanawake Tanzania.

Hata hivyo, Kocha wa timu hiyo, Ahmed Ramadan anamtazama Ubamba kama mchezaji muhimu kwenye kikosi chake kwani ana uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali eneo la kiungo na hata winga wa pembeni.

“Ni mchezaji mzuri sana ambaye kocha yeyote atapenda kumtumia, ana kipaji lakini kuna vitu anapaswa kuongeza,” alisema Ramadan akimzungumzia nyota huyo.

Related Posts