Sultan apata ushindi wa pili Alliance

BAADA ya kupewa kandarasi ya mwaka mmoja na Alliance Girls kama Kocha Mkuu, Sultan Juma amepata ushindi wa kwanza wa ligi wa mabao  5-1 dhidi ya Mlandizi Queens.

Alliance imecheza mechi saba za ligi ikitoa sare mbili, ikishinda mbili dhidi ya Mlandizi na Bunda Queens ikiitandika mabao 2-0 ikipoteza tatu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sultan alisema kama kocha anafurahi kupata ushindi wake wa kwanza akiwa na timu mpya akiamini watakuwa na muendelezo mzuri.

Sultan aliongeza Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu imekuwa ngumu kutokana na ubora wa wachezaji na maandalizi ya timu lakini kama Alliance malengo yao ni kuchukua pointi tatu kila mechi.

“Nimekaa muda mrefu bila ya timu lakini sasa niko na Alliance ambayo imekuwa ikizalisha wachezaji wengi wa kike wanaotumika ndani na nje ya Tanzania na kama kocha natamani kuandika historia nikiwa na timu hii,” alisema Sultan.

Kocha huyo msimu uliopita alitimuliwa na Geita Queens baada ya kufanya vibaya ikishuka daraja.

Related Posts